Makamo katibu mkuu wa mazaru za kishia ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Asubuhi ya siku ya Ijumaa (7 Jamadal-Uula 1442h) sawa na tarehe (23 Desemba 2020m), makamo katibu mkuu wa mazaru za kishia hapa Iraq Shekh Khalifa Jauhar ametembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kufanya ziara na kusoma dua alikwenda katika ukumbi wa utawala wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kukutana na mjumbe wa kamati kuu Sayyid Mustwafa Dhiyaau-Dini na kundi la viongozi.

Shekh Jauhar ameonyesha kufurahishwa na kikao hicho na ametoa shukrani nyingi kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya kutokana na kazi kubwa inazofanya, sambamba na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na watumishi wa Ataba kwa kuhudumia mazuwaru watukufu, akamuomba Mwenyezi Mungu awajalie kila la kheri na mafanikio.

Naye Sayyid Dhiyaau-Dini amezungumza kuhusu umuhimu wa kudumisha mawasiliano na ushirikiano kati ya Ataba tukufu na mazaru takatifu, katika kutekeleza lengo kuu linalo tuunganisha la kuwatumikia maimamu watakatifu (a.s) pamona na familia zao, na kutoa huduma kwa mazuwaru watukufu,

Mwishoni mwa ziara Mheshimiwa akaagwa kama alivyo pokewa, akaombewa arudi salama kama alivyo kuja na kukubaliwa ziara yake za ibada zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: