Toleo la kumi na tano la jarida la Ghadhwiriyya

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa toleo la kumi na tano la jarida la Ghadhwiriyya, lenye kurasa mia moja na kumi na sita, yameandikwa mambo ya kihistoria yanayo husu turathi za Imamu Hussein (a.s), kuanzia watu walio muunga mkono na matukio yake.

Tumeongea na Dokta Ihsani Gharifi kuhusu toleo hilo amesema kuwa: “Jarida hili limeandikwa na kundi la waandishi wa vitabu walio bobea katika kuandika habari za turathi, jarida la Ghadhiriyya lipo wazi kwa kila mtu anaye andika kuhusu turathi za Karbala, tunaamini kuwa waandishi wataandika mada tofauti, kurasa zake zitaonyesha uzowefu wa watu wengine kielimu na kitamaduni, chini ya uzowefu mkubwa wa wasimamizi wake.

Tambua kuwa jarida la Ghadhwiriyya ni jarida la kitamaduni linalo tegemewa na waandishi wengi wa kiiraq limefika toleo la (1621), lilianza kutolewa tangu mwaka 2015m/ 2016 hadi sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: