Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake inajitahidi kuwapa furaha mayatima na wazee

Maoni katika picha
Watumishi wa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, wameratibu program inayo saidia kuingiza furaha kwa mayatima, masikini na wazee wa mkoa wa Najafu, program hiyo ni sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa jua la Zainabiyya kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s).

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika harakati zilizofanywa katika wiki ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa jua la Zainabiyya awamu ya kwanza zilikuwa na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni kutembelea nyumba za kutunzia wazee katika mkoa wa Najafu na kuwapa zawadi pamoja na kuwakumbusha tukio hili adhim, kama sehemu ya kujaribu kuingiza furaha katika nafsi zao”.

Akaongeza kuwa: “Wakati huohuo tuliandaa ratiba ya kutembelea watoto mayatima na masikini pamoja na familia zao, kwa kushirikiana na kituo cha Muhsin, cha utamaduni wa watoto katika Atabatu Alawiyya tukufu, ratiba hiyo ilihusisha kusafiri nao na vipengele vingine, kulikuwa na michezo ya viungo na akili sambamba na mashindano mbalimbali, aidha kulikuwa na maigizo na ugawaji wa zawadi kwa waliofanya vizuri, vilevile kulikuwa na vipindi vya mawaidha chini ya anuani isemayo (malezi ya yatima katika Quráni tukufu) mawaidha yalijikita katika kueleza mwenendo wa Quráni tukufu katika kulea mwanaadamu na kurekebisha jamii, na kukumbusha nafasi ya bibi Zainabu (a.s) aliye simama imara kulea mayatima baada ya vita ya Twafu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: