Ufunguzi wa awamu ya kumi na nne ya kongamano la huzuni za Fatwimiyya

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya Alasiri ya leo siku ya Jumamosi mwezi (10 Jamadal-Uula 1442h) sawa na tarehe (26 Desemba 2020m) ndani ya uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, wamezindua ratiba ya kongamano la kumi na nne katika makongamano ya huzuni za Fatwimiyya, ambalo ni sehemu ya kuadhimisha matukio ya Ahlulbait (a.s) na kukumbuka kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s), litaendelea kwa muda wa siku kumi, ufunguzi huo umehudhuriwa na viongozi wa Ataba mbili tukufu pamoja na kundi la mazuwaru.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo bwana Riyadhu Ni’mah Salmaan amesema kuwa: “Kongamano hili litakuwa na mambo mengi likiwemo igizo kuhusu maisha ya bibi Zaharaa (a.s), litakua na sehemu sita zifuatazo:

  • - Kwanza ni kuhusu utakasifu wake na hadithul-kisaa Alyamaniy.
  • - Pili kuhusu Mtume (s.a.w.w) kuapizana na wakristo wa Najrani.
  • - Tatu kuhusu nyumba ya Zaharaa (a.s) nyumba ya wahyi na utume.
  • - Nne kuhusu khutuba ya Zaharaa (a.s) katika msikiti wa Mtume (s.a.w.w).
  • - Tano tukio la kuvamiwa nyumba ya bibi Fatuma (a.s) na kunjwa ubavu wake.
  • - Sita tukio la kifo cha Zaharaa (a.s) na yaliyojiri baada ya kifo chake.

Akaongeza kuwa: “Kwenye kongamano hili vikundi mbalimbali vya watu wa Karbala vinashiriki pamoja na baadhi ya maktaba zimeshiriki kwa kuweka vitabu tofauti vinavyo weza kusomwa na mtu anayekuja kwenye kongamano au zaairu mtukufu”.

Akaendelea kusema: “Ndani ya siku za kongamano hili kutakua na vikao vya usomaji wa mashairi, pamoja na maukibu ya kuomboleza ya wanawake itakayo fanya matembezi kwa kuanzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi kwenye haram ya Imamu Hussein (a.s), wanawake kadhaa watashiriki matembezi hayo wakiwa wamebeba jeneza la kuigiza, pamoja na mawakibu zingine za watu wa Karbala zitafanya matembezi sawa na hayo”.

Akafafanua kuwa: “Miongoni mwa ratiba ya kongamano pia kutakuwa na kupengele cha uchoraji wa watoto wasiozidi miaka kumi, kila mtoto atachora jambo analo fikiria miongoni mwa dhulma alizofanyiwa bibi Zaharaa (a.s) pamoja na kuwapa zawadi za kuwashajihisha kwa ushiriki wao katika ratiba hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: