Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) yamewekwa mapambo meusi na kutanda huzuni

Maoni katika picha
Majonzi na huzuni imetanda katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kuomboleza msiba mkubwa uliotokea kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wapenzi wao baada ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), nao ni msiba wa kufiwa na Fatuma Zaharaa (a.s) –kwa mujibu wa riwaya ya pili- isemayo alikufa mwezi (13 Jamadal-Uula).

Kuta za Ataba tukufu na korido zake zimewekwa mapambo meusi na mabango yaliyo andikwa kufuatia msiba huu mkubwa.

Kama kawaida ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba yenye vipengele vingi, vinavyo endana na mazingira ya afya ya sasa kufuatia kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona, kutakuwa na mihadhara ya kidini na majlisi za kuomboleza msiba huo, sambamba na kujiandaa kupokea mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya mji mtukufu wa Karbala, zinazokuja kumpa pole bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na harakati zingine kuhusu tukio hilo.

Kumbuka kuwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia wanaomboleza msiba huu wa kufiwa na Fatuma Zaharaa (a.s), kuna riwaya tofauti kuhusu tarehe ya kifo chake na sehemu lilipo kaburi lake (a.s), jambo hili linaonyesha kudhulumiwa kwake na mitihani aliyo kutana nayo, hadi akamuusia mume wake kiongozi wa waumini Ali (a.s) afiche sehemu ya kaburi lake na jeneza lake lisishuhudiwe na mtu yeyote miongoni mwa wale walio mdhulumu, alikufa akiwa na umri wa miaka kumi na nane kwa mujibu wa riwaya mashuhuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: