Kitengo cha Dini kinaomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) na kuangazia nafasi yake katika jamii.

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa ratiba ya kuomboleza inayo tekelezwa kila siku asubuhi ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kukumbuka kifo cha bibi Zaharaa (a.s), kilicho tokea katika siku kama hizi, kwa mujibu wa riwaya ya pili inayo sema alifariki mwezi kumi na tatu Jamadal-Uula, inatolewa mihadhara kuhusu nafasi muhimu aliyokuwa nayo mama huyo mtakasifu katika jamii.

Mzungumzaji ni Shekh Muhsin Asadi kutoka kitengo cha Dini, majlisi hufanywa asubuhi na kuhudhuriwa na mazuwaru pamoja na waombolezaji wa msiba huo, Shekh Asadi anazungumza utukufu wa bibi Zaharaa (a.s) na nafasi yake katika jamii, namna alivyo kuwa nguzo madhubuti katika kusimamia misingi ya Dini, pamoja na kufariki kwake (a.s) akiwa na umri mdogo, tambueni ataendelea kuwa shule kwa vizazi na vizazi na mwanga unaozuwia kila anayetaka kuzima mafundisho ya Dini.

Akafafanua kuwa umma unatakiwa kuchukua mazingatio kutoka kwake (a.s) kama unavyo chukua mazingatio kutoka kwa watoto wake watakasifu (a.s) namna walivyo pigania uislamu, hakika wao ni mfano bora wa kila jambo katika maisha, na mama huyu mtakasifu (a.s) ni kiigizo chema kwa kila mwanamke bali hadi kwa wanaume.

Shekh Asadi alikua anatoa ushahidi wa maneno yake ndani ya Quráni na hadithi za Mtume pamoja na watu wa nyumbani kwake (a.s), kila mhadhara ulihitimishwa kwa tenzi za uombolezaji zinazo onyesha namna alivyo dhulumiwa na jinsi alivyo kufa kishahidi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: