Mawakibu za kuomboleza na mazuwaru wanampa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) tangu asubuhi ya leo mwezi kumi na tatu Jamadal-Uula, imeshuhudia kumiminika kwa mazuwaru kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, pamoja na vikundi vya mawakibu vilivyo kuja kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili.

Rais wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya bwana Riyadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mawakibu za waombolezaji zilizokuja kuomboleza msiba huu zinatoka ndani ya mkoa wa Karbala, kipindi hiki huitwa msimu wa huzuni za Fatwimiyya kwao huwa ni msimu wa Muharam ndogo, hufanya maombolezo mbalimbali karibu na siku za kifo chake na huendelea hadi baada ya tarehe aliyo fariki, huweka mapambo meusi njiani na barabarani pamoja na kufanya majlisi za kuomboleza katika Husseiniyya, na matembezi ya kuomboleza ambayo huanzia katika moja ya barabara inayo elekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuingia katika malalo hiyo takatifu kisha kuelekea katika malalo ya Imamu Hussein (a.s), kwa kupitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Kitengo kimeandaa ratiba inayo endana na mazingira ya sasa, pamoja na kusimamia matembezi ya mawakibu hizo ili kuepusha muingiliano kati ya mawakibu na mazuwaru”.

Tambua kuwa hakuna tarehe maalum ya kifo chake (a.s), kuna riwaya tatu tofauti kuhusu tarehe hiyo baada ya Mtume (s.a.w.w), kwa hiyo kila mwaka waislamu huomboleza kifo chake kwa kufuata riwaya zote tatu, kila tarehe huitwa (msimu wa huzuni za Fatwimiyya).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: