Majlisi ya kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Katika kuhuisha kifo cha mbora wa wanawake duniani bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili, idara ya wahadhiri wa Husseiniyya wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi maalum ya wanawake kuomboleza msiba huu kwa mwaka wa tano mfululizo.

Makamo kiongozi wa idara hiyo bibi Taghridi Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Idara yetu imekuwa ikiomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kwa kufanya majlisi ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika sardabu ya Imamu Kadhim (a.s), huanza kwa kutoa mhadhara kuhusu utukufu wa bibi Zaharaa (a.s) kisha hufanya igizo linalo onyesha namna alivyo dhulumiwa (a.s), majlisi hizi zina athari kubwa kwa wahudhuriaji na kwa watoto pia na ndio sababu ya kuendeleza swala kili kila mwaka”.

Akaongeza kusema: “Tumezingatia kanuni za afya katika ukaaji na kuvaa barakoa na soksi za mikononi pamoja na kupuliza dawa, majlisi hizi zinafanywa kwa kushirikiana na maktaba ya Ummul-Banina (a.s) na wakina dada wa Zainabiyaat”.

Kumbuka kuwa idara ya wahadhiri wa kike huwajibika kufanya majlisi za kuomboleza vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), na itafanya majlisi kama hii kwa mujibu wa riwaya ya tatu pia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: