Kuanza mkutano wa makabila chini ya kongamano la kuomboleza la mwaka wa kumi

Maoni katika picha
Asubuhi ya Jumatano mwezi (14 Jamadal-Uula 1442h) sawa na tarehe (30 Desemba 2020m), umefanyika mkutano wa makabila chini ya kongamano la mwaka wa kumi, linalo simamiwa na taasisi ya Imamu Hussein (a.s) na idara ya Mawakibu Husseiniyya katika mtaa wa Dabuni mkoani Waasit kwa kushirikiana na Ataba ya (Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya, Abbasiyya pamoja na kamati ya Hashdu-Shaábi, kwa ajili ya kuhuisha na kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa a.s).

Mkutano huo umepata mahudhurio makubwa ya viongozi wa makabila na dini kutoka mtaa wa Dabuni, ratiba ya mkutano huo imehusisha ufunguzi wa maonyesho ya vitabu ambayo Atabatu Abbasiyya tukufu imekua na ushiriki mkubwa.

Siku ya kwanza ya kongamano imezungumzwa nafasi ya makabila ya Iraq katika kushikamana na mwenendo wa bibi Fatuma na kufanyia kazi mafundisho ya Mwenyezi Mungu.

Kumbuka kuwa kongamano la kuomboleza ambalo hufanywa kila mwaka, litafanywa Ijumaa ijayo, likitanguliwa na vikao vingi vya kujadili mambo tofauti yanayo lenga kusimamia misingi ya dini, akhlaq na malezi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: