Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kimeratibu semina ya hati za kiarabu

Maoni katika picha
Katika muendelezo wa semina za hati za kiarabu na mapambo yake pamoja na kuhakiki khutuba na lugha ya kiarabu, kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeratibu semina kuhusu hati za kiarabu, kwa lengo la kuenzi fani hiyo tukufu, na kuendeleza kipaji cha uandikaji kwa watumishi wake.

Mkufunzi wa semina hiyo alikuwa ni Amiir Karbalai mmoja wa wataalamu wa hati katika idara ya (Turathi nzuri), itaendelea kwa muda wa siku kumi na moja, kila siku kutakuwa na mhadhara mmoja.

Msimamizi wa semina amesema kuwa: “Semina inalenga kuangazia fani hii tukufu, na kubainisha mambo ambayo muandishi hukusudia kuyafikisha kwa jamii kwa kutumia fani hiyo”.

Akaongeza kuwa: “Hali kadhalika semina inalenga kuandaa waandishi kwa kufuata misingi sahihi na kujitenga na uholela katika kusomesha na kusoma, na kuhimiza kuheshimiwa kwa misingi ya hati ya kiarabu yenye umuhimu mkubwa, na inayo takiwa muandikaji aifuate na kulinda isipotee”.

Akafafanua kuwa: “Tunafanya kila tuwezalo ili kuifanya semina hii iwe na uwanja mpana kwa watu wa mkoa wa Karbala na mikoa mingine ya Iraq, kwa kusambaza utamaduni wa hati za kiarabu pamoja na kunufaika na teknolojia za kisasa katika uandishi wa herufi za kiarabu”.

Tambua kuwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kinaendelea kufanya semina na warsha za kujenga uwezo, kwani ni moja ya vitengo muhimu vyenye jukumu la kuhuisha turathi za kiislamu na kuonyesha thamani yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: