Kituo cha (Ruhamaau-Bainahum) kimepokea watoto 300 waliokosa malezi ya familia na kimeandaa utaratibu wa kuwalea na kuwaingiza katika jamii

Maoni katika picha
Kikosi cha kituo cha (Ruhamaau-Bainahum) chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kimepokea kundi la kwanza la watoto waliokosa malezi ya familia, jumla ya watoto (300) huku (50) kati yao wakitoka mkoa wa Karbala, na wamepokelewa kwa awamu baada ya kumaliza kukagua mitaa, hii ndio idadi kubwa tangu kufunguliwa kwa kituo hiki zaidi ya miaka mitatu iliyopita, kituo kitaandaa utaratibu kamili wa kuwaandaa na kuwaingiza katika jamii na kuwa mfano mwema kwa wenzao.

Mkuu wa kituo hicho Ustadh Amiri Hassan ameongea na mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ndoto ya kituo ni kutengeneza watu bora katika jamii, hivi karibuni tumeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watoto, chini ya maelekezo ya Atabatu Abbasiyya na kiongozi mkuu wa kisheria umewekwa utaratibu maalum wa kuwapokea na kuwaingiza katika orodha ya kituo, pamoja na kufanya makubaliano maalum na walezi wao kisha kuanza kuwapa mafunzo, chini ya mazingira maalum yanayo endana na hali ya tahadhari ya maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akaongeza kuwa: “Tutatoa mafunzo ya malezi elimu na afya pamoja na ufundi na kuwapa misaada inaowafaa, mafunzo yote yanatolewa na walimu mahiri waliobobea katika fani hizo, na kuwawezesha kujitegemea na kutumikia jamii na taifa lao kwa kupikia malengo yafuatayo:

  • - Kuboresha malezi na elimu.
  • - Kutoa msaada wa kiafya na kisheria.
  • - Kuendeleza vipaji.
  • - Kuandaa makazi bora ya watoto”.

Tambua kuwa kituo kimefanikisha mambo yafuatayo:

  • - Kukutanisha watoto 26 na familia zao na kuwapa mahitaji yote muhimu katika maisha yao, pamoja na kuwaandikisha katika shule za Al-Ameed ambapo wanasoma bure.
  • - Kutoa uangalizi kwa watoto 34 na kuwaandikisha katika shule za Al-Ameed, pamoja na kutengeneza furaha kwa watoto zaidi ya 200 kwa kuwapa baadhi ya mahitaji muhimu yanayo ingiza furaha katika nyoyo zao.
  • - Kuanzisha (Ruhamaau-Bainahum/ kitengo cha wanawake) kwa ajili ya kulea watoto wa kike.
  • - Kuanzisha kikosi cha (mtoto mpole) kwa ajili ya kutoa misaada chini ya usimamizi wa watoto baada ya kuwawezesha.

Kumbuka kuwa kituo cha (Ruhamaau-Bainahum) kinaendeshwa na vijana chini ya anuani isemayo: (muelekezaji wa kheri sawa na mtendaji wake), nao ni mradi wa kiiraq ulioanzishwa katika mji wa Karbala, unaolenga kuokoa maisha ya watoto (wakiume na wa kike) wasipotee na kuingia katika makundi mabaya, mradi huu umepata ufadhili wa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, na unafanya kazi chini ya uangalizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: