Huzuni za Fatwimiyya katika uwanja wa chuo kikuu cha Al-Ameed

Maoni katika picha
Kitengo cha kuongoza nafsi na malezi katika chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeandaa hafla ya kuomboleza kifo cha Ummu-Abiha bibi Zaharaa (a.s), katika ukumbi mkuu na kuhudhuriwa na wakufunzi pamoja na kundi kubwa la wanafunzi wa chuo.

Hafla hiyo imefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na mmoja wa wanafunzi wa chuo, ukafuata mhadhara wa Shekh Muhammad Kuraitwi kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, amezungumza mambo muhimu katika historia ya bibi Zaharaa (a.s), akafafanua kuwa: “Ukiangalia historia yake pamoja na kuishi miaka michache lakini imejaa mafunzo katika kila sekta ya maisha, hakika yeye ni kiigizo chema kwa kila mwanamke bali hadi kwa wanaume”.

Akafafanua nafasi yake katika uislamu na kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu wakati wa baba yake na wakati wa mume wake, akaeleza sifa zake (a.s) zilizo mfanya kuwa mwanamke bora katika zama zake, miongoni mwa sifa alizokuwa nazo na zinazotakiwa kuwa somo kwa jamii zote na umma kwa ujumla ni zuhudi (uchamungu) ukarimu, kujitolea, subira pamoja na zingine nyingi, alikuwa na ikhlasi katika ibada zake, alizifanya kwa Imani ya hali ya juu, moyo wake ulijaa Imani ya hali ya juu, aidha akaeleza sifa tukufu za bibi Zaharaa (a.s) zilizo tajwa ndani ya Quráni tukufu na hadithi za Mtume na Maimamu, akamaliza mhadhara kwa kusoma tenzi iliyo eleza namna alivyo dhulumiwa na matatizo aliyopata baada ya kifo cha baba yake (s.a.w.w).

Baada ya hapo ukaingia wakati wa mashairi ya Husseiniyya yaliyo somwa na mtumishi wa chuo, hafafu yakafuata maswali ya kidini na kutoa zawadi kwa wale waliojibu vizuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: