Maahadi ya Quráni tukufu inafanya mashindano ya kuhifadhi

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kupitia tawi lake la wilaya ya Hindiyya, inafanya mashindano ya kuhifadhi Quráni yanayo husisha wanafunzi walioshiriki kwenye semina za tahfiidh, ili kuwawezesha kuhifadhi vizuri na kuwatia moyo wa kuendelea kuhifadhi.

Kiongozi wa tawi hilo Sayyid Haamid Marábi amesema kuwa: “Hakika mashindano ya Quráni, sawa yawe ya kuhifadhi au aina nyingine ni sehemu muhimu ambayo hufanywa na Maahadi pamoja na matawi yake, na shindano hili ni sehemu ya mashindano hayo, limefanywa kwa kufuata masharti yote ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akaongeza kuwa: “Hili ni shindano la kwanza kufanywa na Maahadi baada ya kuanza kufanya shughuli zake zilizo simama kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akabainisha kuwa: “Washiriki wa shindano ni wale walio hifadhi kuanzia juzuu tano za Quráni tukufu, kuna utaratibu maalum ambao unafatwa kuwapata washindi, washiriki wamechuana vikali na hatimae wakapatikana washindi sita, wiki ijayo watashiriki kwenye awamu ya mwisho na atapatikana mshindi mmoja”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: