Kongamano la shahada la awamu ya kumi limehitimisha ratiba yake

Maoni katika picha
Kitongoji cha Dabuni katika mkoa wa Waasit kimehitimisha awamu ya kumi ya kongamano la shahada, linalo simamiwa na taasisi ya Imamu Hussein (a.s) na idara ya mawakibu za Husseiniyya katika kitongoji hicho, kwa kushirikiana na Ataba za (Alawiyya, Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya) pamoja na kamati ya Hashdu-Shaábi katika kuhuisha na kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s).

Kongamano limedumu kwa muda wa siku tatu na lilikuwa na vitu tofauti, kulikuwa na maonyesho ya vitabu ambayo Ataba tukufu zimeshiriki, likiwemo tawi maalum la kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, aidha kulikuwa na mkutano wa makabila pamoja na mkutano wa wanawake, hali kadhalika imetangazwa kuanzishwa jukwaa la vijana la kujadili mambo yanayo husu vijana, pamoja na mihadhara na nadwa za mafunzo elekezi, vipengele vyote vya kongamano hilo vimepata muitikio mkubwa kutoka kwa viongozi wa dini, utamaduni na sekula, na wawakilishi wa Ataba tukufu ya Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya, Abbasiyya, na vikundi vingine vya kijamii kutoka ndani na nje ya mkoa.

Hafla imefunguliwa kwa Quráni tukufu, ukafuata ujumbe wa Muútamad Marjaiyya Shekh Swalehe Qarghuli, akatoa shukrani kwa wasimamizi wa kongamano hili ambalo linafanywa kwa mwaka wa kumi mfululizo, halafu ukafuata ujumbe wa Sayyid Izu-Dini Alhakiim, akabainisha nafasi ya bibi Zaharaa (a.s) katika kulinda haki ya kiongozi wa waumini (a.s) na akaeleza upotoshwaji uliofanywa baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), na kwamba yeye aliubainishia umma mustaqbali wanao subiri baada ya kuacha usia wa Mtume (s.a.w.w).

Hafla ya kufunga kongamano ikapambwa na mashairi pamoja na maigizo, mwisho kabisa wahudhuriaji wakapewa vyeti vya ushiriki, pamoja na kugawa zawadi kwa washindi wa mashindano yaliyo fanywa wakati wa kongamano pamoja na kugawa zawadi kwa baadhi ya familia za mashahidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: