Katika kumbukumbu ya kifo cha mama wa baba yake: chuo kikuu cha Alkafeel kinakumbuka historia ya Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kimefanya kumbukumbu ya kifo cha mama wa baba yake bibi Zaharaa (a.s), kwenye ukumbi mkuu wa chuo na kuhudhuriwa na rais wa chuo Dokta Nuris Muhammad Shahidi Dahani na msaidizi wake, pamoja na wakuu wa vitivo, wakufunzi na watumishi.

Majlisi imefunguliwa kwa Quráni tukufu ukafuata mhadhara uliotolewa na Shekh Abdullahi Dujaili, amezungumzia nafasi tukufu ya bibi Zaharaa (a.s) mbele ya baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) hadi akasema: (Fatuma ni pande la mwili wangu na mimi ni sehemu yake, atakae muudhi ameniudhi mimi na atakae niudhi, amemuudhi Allah), utukufu kama huo haujathibiti kwa mtu mwingine yeyote tofauti na Fatuma (a.s).

Akataja dhulma kubwa aliyo fanyiwa bibi Zaharaa (a.s) baada ya kufa baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), alipata maudhi ya kiroho na kimwili, alichomewa nyumba yake na kuvunjwa mbavu yake na kutoka mimba pamoja na kunyimwa mirathi ya baba yake na hata mali aliyopewa na baba yake.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Alkafeel huadhimisha matukio yanayo wahusu Ahlulbait (a.s), ya kuzaliwa na kufa chini ya ratiba maalum, na hualikwa wahadhiri na wasomi kwenye maadhimisho hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: