Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) ya wahadhiri wa kike inafanya mitihani yake ya majaribio

Maoni katika picha
Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) ya wahadhiri wa Husseiniyya wakike katika Atabatu Abbasiyya imetoa mtihani baada ya kuwafundisha kwa njia ya mtandao, kutokana na kuwepo kwa janga la virusi vya Korona na kuheshimu maelekezo ya idara ya afya.

Makamo kiongozi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya Ustadhat Taghrida Abdulkhaliq Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maahadi imeanza kutoa mitihani ya kila mwezi kwa wanafunzi wake baada ya kumaliza mada zilizo pangwa katika mwezi wa kwanza kwa hatua zote, ya kwanza, ya pili na ya tatu, pamoja na kozi za (Nuru Zaharaa) na (Albatuli), mitihani imefanywa chini ya tahadhari kubwa ya kujikinga na maambukizi na kulinda usalama wa wanafunzi”.

Akabainisha kuwa: “Huu ni mtihani wa kwanza baada ya kuanza kufundisha kwa kutumia mitandao, masomo yameendelea kama kawaida lakini kutokana na mazingira ya afya pamoja na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuhakikisha masomo yanaendelea bila kusimama, tumeamua kufundisha kwa kutumia mtandao ya mawasiliano (telegram)”.

Akasisitiza kuwa: “Matokeo ya awali ya mtihani huo yanaonyesha masomo yaliyofundishwa kwa njia ya mtandao yameeleweka vizuri, jambo hili linaonyesha kuwa ufundishaji umekuwa na mafanikio makubwa, wakufunzi wameweza kufafanua masomo vizuri na kwa njia inayo eleweka kwa urahisi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: