Atabatu Abbasiyya tukufu imerudisha uhai kwenye maktaba ya chuo cha Imamu Kaadhim (a.s) katika mkoa wa Baabil

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya imerudisha uhai kwenye maktaba ya chuo cha Imamu Kaadhim (a.s) tawi la mkoa wa Baabil, chini ya utaratibu wa kusaidia vyuo vya Iraq viweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi, maktaba za chuo ni moja ya sehemu muhimu katika uboreshaji wa elimu.

Kazi hiyo imefanywa kwa kushirikiana na idara ya uhusiano na vyuo vikuu na shule katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Ustadh Hussein Shaakir msimamizi wa kazi hiyo amesema kuwa, baada ya Atabatu Abbasiyya tukufu kupokea maombi ya kukarabati maktaba, kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi aliagiza kuanza kuweka vifaa katika maktaba pamoja na vitabu mbalimbali”.

Akaongeza kuwa: “Kitengo cha majengo ya kihandisi kimetengeneza kabati mpya za vitabu zenye muonekano wa kisasa, mafundi selemala walichukua vipimo na kuandaa kila kinacho hitajika kwenye ujenzi huo, halafu wakaanza kutengeneza kama ilivyo pangwa na kamati ya mafundi selemala, baada ya kumaliza kutengeneza kabati hizo zimewekwa kwenye ukumbi wa maktaba na kurudia muonekano wa zamani, na kuifanya iendane na vitavu ilivyo navyo”.

Idara ya maktaba imepokea kwa furaha mradi huu na imesema kuwa hili sio jambo geni kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwani imesimama mstari wa mbele kusaidia miradi au taasisi zinazo toa huduma kwa wananchi, ikiwemo sekta hii ya maktaba.

Kumbuka kuwa kutakuwa na ufunguzi rasmi wa maktaba utakaofanywa kwenye vitengo vya chuo, kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu siku zijazo Insha-Allah.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: