Maadalizi ya idara ya mahusiano ya vyuo na shule ya kuandaa mkutano kwa ajili ya Karbala ya kielektronik

Maoni katika picha
Miongoni mwa maandalizi ya idara ya mahusiano ya vyuo na shule ya kuandaa mkutano kwa ajili ya Karbala ya kielektronik, ugeni na muwakilishi wa kitengo cha maandalizi na mafunzo kutoka idara kuu ya malezi mkoa wa Karbala umekwenda Bagdad kutoa mualiko maalum wa mkutano huo.

Ugeni huo umewasili katika wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu na kukutana na kiongozi wa idara ya tafiti na maendeleo pamoja na rais wa kitengo cha miradi ya kibunifu, na mkuu wa chuo cha ibun Haithami na rais wa kitengo cha kompyuta.

Kisha ugeni huo ukaenda wizara ya malezi na kukutana na mkuu wa ofisi ya waziri pamoja na kiongozi mkuu wa program na idara ya maandalizi na mafunzo.

Aidha wamekutana na katibu mkuu kiongozi msaidizi wa ofisi pamoja na kiongozi wa elimu za kielektronik na idara ya habari ya waziri.

Mwisho wa ziara yao wawasilisha mualiko wa kikoa kutoka idara ya mahusiano katika mkoa mtukufu wa Karbala.

Kumbuka kuwa kikao hicho kitafanywa katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa njia ya mtandao siku ya Jumamosi asubuhi (9/1/2021m) kupitia program ya Zoom, na kurushwa moja kwa moja katika ukurasa wa mradi wa kijana mzalinde wa Alkafeel wa facebook kuanzia saa (9:00).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: