Mkuu wa mkoa wa Najafu amefanya ziara katika Atabatu Abbasiyya tukufu na amekutana na katibu mkuu na kusifu huduma zinazotolewa na Ataba kwa mazuwaru

Maoni katika picha
Mkuu wa mkoa wa Najafu Sayyid Luay Alyaasiri amesifu huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru wanaokuja kutembelea malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na miradi mikubwa wanayo fanya ya kuhudumia wananchi wa Iraq.

Ameyasema hayo alipo tembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kuzuru kaburi takatifu la Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kumaliza ibada ya ziara amekutana na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo.

Mheshimiwa Alyaasiri amesikiliza maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru, na zile zinazo tolewa kwa wananchi. Mwisho wa ziara yake Sayyid Alyaasiri akaushukuru uongozi wa Atabatu Abbasiyya na watumishi wake kwa kazi kubwa wanayo fanya ya kuhudumia malalo takatifu na mazuwaru, akawatakia mafanikio mema katika kazi zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: