Kuanza kwa kikoa cha kongamano la teknolojia kwa ajili ya Karbala

Maoni katika picha
Asubuhi ya Jumamosi mwezi (24 Jamadal Uula 1442h) sawa na tarehe (9 Januari 2021m) vimeanza vikao vya kongamano la teknolojia kwa ajili ya Karbala, linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala, linalenga kuchangia maarifa ya msingi katika kutumia mitandao ya mawasiliano ya kijamii kwenye ufundishaji.

Kongamano linafanyika ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kuhudhuriwa na wawakilishi wa wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu pamoja na wizara ya malezi na wawakilishi kutoka vyuo vikuu mbalimbali na wadau wa sekta hiyo kutoka taasisi tofauti za serikali na binafsi.

Kongamano limefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na Ammaar Hilliy kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq halafu ukafuata wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu (Lahnul-Ibaa).

Kisha ukawasilishwa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Ahmadi Kaábi, aliye anza kwa kufikisha salamu za kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya na katibu mkuu kwa wasimamizi wa kongamano hili na kuwatakia mafanikio mema yatakayo saidia kusukuma kurudumu la elimu sambamba na kuhimiza umuhimu wa kuunganisha nguvu hasa kwa taasisi za serikali na kuhakikisha raia wanapata huduma bora, kufanya kazi kwa pamoja huwa na matokeo mazuri daima.

Idara ya malezi ya mkoa wa Karbala imewasilisha mada kwenye kongamano hili, iliyo tolewa na kiongozi wake Ustadh Abbasi Auda, akasema kuwa: mwanaadamu anapokuwa mahala fulani anahitaji kutafakari na kuchukua maamuzi, tulipojikuta kwenye mazingira magumu kama wizara ya malezi na elimu ya juu tuliona kuwa hatuwezi kusimama kwenye jambo moja peke yake katika ufundishaji, bali ilikua ni muhimu kutumia njia mbalimbali ikiwemo teknolojia katika utoaji wa elimu.

Ratiba ya kongamano ikaendelea kwa kuwasilishwa mada mbalimbali za kielimu kama ifuatavyo:

  • - Hali ya utumiaji wa teknolojia katika wizara ya elimu ya juu / Dokta Aamir Salim Amiir mhusika wa mafunzo ya teknolojia/ katika wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.
  • - Ubadilishaji wa namba Dokta Yusufu Khalaf Yusufu mkuu wa kitengo cha miradi katika wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.
  • - Mustakbali wa mashirika ya Iraq na usalama wake/ Dokta Hamuud Shukru Mahmuud/ muwakilishi wa shirika la Cisco hapa Iraq/ kutoka chuo kikuu cha Mansuur.
  • - App za shirika la Google zinazotumika kufundishia kwa njia ya mtandao/ Dokta Adiy Ali Ahmadi/ mkuu wa kituo cha njia tofauti za ufundishaji wa kielektronik.
  • - Kujenga uwelewa kwa mtu na jamii kuhusu makosa ya kimtandao ili kujiweka salama/ Ustadh Muhammad Mardani Mahmuud/ mtaalam wa makosa ya mitandaoni.

Kongamano litaendelea leo baada ya Adhuhuri kumalizia uwasilishwaji wa mada kisha kuandaa maazimio na yatokanayo na kongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: