Kikao cha uwajilishwaji wa mada: kuhitimisha ratiba ya kongamano la (Teknolojia kwa ajili ya Karbala)

Maoni katika picha
Jioni ya Jumamosi ya leo mwezi (24 Jamadal-Uula 1442h) sawa na tarehe (9 Januari 2021m), imehitimishwa ratiba ya kongamano la (Teknolojia kwa ajili ya Karbala) lililo andaliwa na Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala na kufanywa katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s).

Ratiba ya jioni imeshuhudia uwasilishwaji wa mada zinazo lenga kuboresha ufundishaji kwa njia ya mtandao hapa Iraq, mada zilizo wasilishwa ni:

Mada ya kwanza: mahitaji ya kubadilika na kuwa miji endelevu na njia za kufanikiwa/ Dokta Haid Al-Ameed/ kiongozi wa serikali na ujenzi wa serikali mtandao na mabadiliko ya namba katika mataifa ya falme za kiarabu (Imaraat).

Mada ya pili: ratiba ndogo/ Ali Aadil Ali Azubaidi/ kutoka wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu ofisi ya kusimamia viwango vya elimu kwa kushirikiana na Dokta Mustwafa Khalidi Mazáli mkuu wa shirika la (AiNi) la taaluma za kiteknolojia.

Mada ya tatu: hali ya mafunzo ya teknolojia katika wizara ya malezi/ Waaili Wahidi Shati kiongozi wa idara ya elimu za kielektronik katika idara kuu ya selebasi.

Mada ya nne: program za kielektronik zilizo tengenezwa na raia wa Iraq/ Wasam Ali Khuzaaiy/ kituo cha Alkafeel cha taaluma ya teknolojia.

Mada ya tano: kunufaika na muendelezo wa namba katika program za kitamaduni (mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel kama mfano) Maahir Khalid Almayahi/ kiongozi wa idara ya uhusiano wa vyuo na shule katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mada ya sita: matumizi ya App katika kazi za kiidara/ Ustadh Farasi Abbasi Hamza/ kiongozi wa idara ya mawasiliano/ kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: