Kituo cha Multaqal-Qamaru kinafanya harakati kubwa katika mkoa wa Misaan

Maoni katika picha
Kikosi cha kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya harakati mbalimbali katika mkoa wa Misaan, zinazo lenga makundi tofauti ya vijana kwa ajili ya kuwajengea uwezo na taaluma na kuwafanya kuwa watu wenye athari katika jamii, sambamba na kuibua changamoto pamoja na kuzitafutia ufumbuzi, na kuwatenga na mambo mabaya yanayo anza kuenea hapa Iraq.

Haya yamesemwa na kiongozi wa kituo hicho Shekh Haarith Daaji, akaongeza kuwa: “Harakati za kituo hazijaishia kwenye kukusanya makundi ya vijana kutoka mikoa tofauti peke yake, kuna harakati zingine zinazo endelea kwenye mitandao, na safari ya mkoa wa Misaan ni moja ya harakati hizo, miongoni mwa mambo yaliyo fanywa ni:

  • - Tumefanya warsha tatu kwa vijana wa mji wa Ammaarah, kwenye msikiti wa mtaa wa Askariy, warsha hizo zilikuwa na maudhui tofauti zenye lengo moja la kuwafanya vijana waweze kupambana na changamoto zinazo wazunguka, warsha hizo zilikua na anuani zisemazo (kuongoza nafsi – kujenga itikadi – taqlidi na marjaiyyah).
  • - Kufanya kikao na wawakilishi wa vituo vya hapa mkoani, na kujadili mambo mbalimbali yanayo lenga kuboresha utendaji katika mkoa.
  • - Tumefanya warsha tatu kwa kundi kubwa la vijana wa wilaya ya Kahalaa ndani ya chuo kikuu cha Kahalaa zilizo kua na anuani zisemazo (mawimbi ya kubadilika jamii na athari yake katika kujenga misingi ya vijana – nidhamu ya dhati – utamaduni bora).
  • - Tumefanya kikao kikubwa na vijana wa kitongoji cha Musharaha, na kufanya warsha mbili, moja ilikua na anuani isemayo misingi ya mafanikio, na nyingine uwezo na uwajibikaji”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: