Kuanza kwa ratiba ya hema la Qassim (a.s) ya kufundisha uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza

Maoni katika picha
Wataalamu wa Alkafeel wa uokozi na huduma ya kwanza ya kitabibu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza semina ya nne baada ya mazowezi hamsini ya uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza ya kitabibu katika hema za mafunzo ziitwazo Qassim bun Imamu Mussa bun Jafari (a.s), na kushiriki wapiganaji wa serikali na Hashdu-Shaábi.

Hema za mafunzo ni muendelezo wa mafunzo mengine yaliyo fanywa, kwa ajili ya kujenga uwezo wa uokozi vitani pamoja na utoaji wa huduma ya kwanza ya kitabibu katika mazingira hatari na kusaidia kupunguza idadi ya vifo.

Kiongozi wa mafunzo ya uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza Dokta Ibrahim Abuu Twahin ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mafunzo katika hema hizi yatafanyika kwa muda wa siku sita kwa nadhariyya na vitendo, ili kuwafanya wanasemina waweze kuelewa masomo vizuri, watafundishwa mbinu za kuokoa majeruhi aliye katikati ya mapambano makali, pamoja na kuhakikisha usalama wa anga, na kusaidia mtu aliye jeruhiwa kifuani na kumpima majeruhi pamoja na kumtoa sehemu hatari”.

Tambua kuwa wataalamu wa Alkafeel wanafundisha mambo yafuatayo:

Kwanza: uokozi vitani na walengwa ni wanajeshi.

Pili: utoaji wa huduma za matibabu na walengwa ni madaktari na wauguzi.

Tatu: usalama wakati wa kazi na walengwa ni watumishi wa mashirika na taasisi mbalimbali.

Nne: jamii ya raia wa Iraq kwa ujumla.

Tano: majanga ya halaiki walengwa ni watumishi wa vitengo vya uokozi.

Kumbuka kuwa wataalamu wa Alkafeel wa uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza wamesha fundisha mamia ya waokozi kutoka vikosi tofauti vya wanajeshi, na kuhitimu mbinu mbalimbali za uokozi baina yao wanapokuwa katikati ya vita na kuokoa nafsi zao takatifu, sambamba na kutoa vyeti kwa wahitimu vinavyo kubalika kitaifa na kimataifa ikiwa ni pamoja na nchi za ulaya (ESA).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: