Makumbusho ya Alkafeel inafanya ukarabati mkubwa katika ukumbi wake wa maonyesho

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha makumbusho ya Alkafeel wanafanya ukarabati mkubwa ndani ya ukumbi wake wa maonyesho, ambao unaturathi adimu zinazo rudi miongo mingi ya zamani, kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya kuhifadhi turathi hizo na kuifanya sehemu zilizopo kuwa na muonekano mzuri ndio sababu ya kufanywa ukarabati huu.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo Ustadh Swadiq Laazim, akaongeza kuwa: “Kazi ya ukarabati ndani ya ukumbi wa maonyesho ya makumbusho au kumbi zingine zilizo chini ya kitengo hiki, hufanya mara kwa mara tena kwa ratiba maalum, lakini kuna ukarabati mwingine hufanywa kwa kina na umakini ya hali ya juu, ukiwemo ukarabati huu, unaofanywa na watumishi wetu ndani ya ukumbi wa maonyesho ya makumbusho, miongoni mwa mambo yanayo fanywa ni:

  • - Kuondoa kapeti la zamani na kutandika jipya lenye rangi nzuri na imara linalo endana na vitu vinavyo onyeshwa.
  • - Kusafisha ukumbi na kukarabati kwa kutumia vifaa maalum.
  • - Kutengeneza na kurekebisha baadhi ya kabati za kuwekea vitu vya maonyesho na kubadilisha zilizo haribika.
  • - Kubadili baadhi ya maeneo na kuyafanya kuwa sehemu mpya za maonyesho.
  • - Kusafisha kila kitu kwa kutumia vifaa maalum chini ya wataalamu waliobobea katika uhifadhi wa mali-kale.
  • - Kupaka rangi upya baadhi ya sehemu zilizo chakaa kwenye kuta na kabati.
  • - Kukarabati njia zote za umeme pamoja na taa zote zilizopo ndani ya ukumbi, na kuondoa zilizo haribika.
  • - Kukarabati jukwaa kuu la maonyesho.
  • - Kukarabati miswala ya maonyesho iliyopo ndani ya makumbusho”.

Akabainisha kuwa: “Kazi hii imechukua siku kadhaa jambo ambalo limepelekea kufungwa makumbusho, baada ya kumaliza matengenezo hayo makumbusho itakua tayali kupokea watu wanaokuja kuitembelea ikiwa katika muonekano mpya”.

Kumbuka kuwa ukumbi wa maonyesho ya makumbusho ya Alkafeel upo upande wa kulia kwa ndani ukitokea mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), nao ni miongoni mwa kumbi za kisasa kuanzia mpangilio wake na mali-kale zinazo onyeshwa kwenye makumbusho hiyo, zimewekwa kwa kufuata utaratibu wa kimataifa, idara ya maktaba inafanya kazi kisasa sambamba na kuendana na maendeleo ya makumbusho duniani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: