Mradi wa kware unazalisha ndege elfu 20 kwa mwezi na umeweka mkakati wa kuongeza uzalishaji

Maoni katika picha
Idara ya mradi wa kware chini ya shirika la uchumi Alkafeel moja ya mashirika ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imesema kuwa inazalisha kware (elfu 20) kwa mwezi, kuna mkakati wa kuongeza uzalishaji kwa kiwango kikubwa ndani ya mwaka huu kulingana na mahitaji ya soko la ndani, kuongeza uzalishaji kunatokana na kukubalika ndege hao katika soko la ndani, ukizingatia kuwa nyama ya ndege hao ni nzuri na inafaida nyingi, mkakati wa kuongeza uzalishaji wa ndege hao ni kufikia kiwango cha mayai (40,000) kwa mwezi.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa shirika hilo Mhandisi Rasuli Ramaah, akaongeza kuwa: “Mradi wa kufuga kware ni mradi pekee Karbala na wakwanza kwa aina hii hapa Iraq, umefanikiwa kuongeza pato la taifa, pamoja na kupunguza haja ya kuagiza ndege hao kutoka nje ya taifa”.

Akabainisha kuwa: “Ufugaji huo unafanywa ndani ya kumbi kubwa nne zenye kila kinacho hitajika, kuna mashine za kutotolesha mayai, sehemu ya kutunzia vifaranga, kila ukumbi unakware jike -mitetea- (6000) ambazo hutaga mayai yanayo kwenda kutotolewa kwenye mashine na mengine huuzwa kwa ajili ya kuliwa”.

Akasema: “Uzalishaji wa kware umefika (20,000) kwa mwezi na huuzwa pamoja na mayai katika vituo vya mauzo vya Alkafeel pamoja na sehemu zingine, huku mayai mengine yakitotoleshwa kwa ajili ya kuongeza wingi wa kware”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inamiradi mingi ya viwanda, kilimo na ufugaji, miradi hiyo imesaidia kupunguza uagizaji wa vitu kutoka nje ya taifa, miongoni mwa miradi yenye mafanikio makubwa ni huu wa ufugaji wa kware, unaofanywa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (10,000) barabara ya (Najafu – Karbala).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: