Uhusiano baina ya daktari na mgonjwa na athari yake katika huduma ya matibabu.. anuani ya mhadhara wa kielimu uliotolewa katika chuo kikuu cha Al-Ameed

Maoni katika picha
Mkuu wa kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Al-Ameed ameandaa mhadhara wa kielimu kuhusu uhusiano wa daktari na mgonjwa na athari yake katika huduma ya tiba hapa Iraq.

Mhadhara umetolewa na mkufunzi wa chuo Dokta Karimu Thaamir Kaábi mbele ya walimu, ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Mhadhara uzungumzia sababu za kijamii, kitamaduni na kisheria ambazo zimekuwa na uweliwa mbaya kwa muda mrefu na mara nyingi kumekuwa na makosa yanayo tokea kati ya daktari na jamii, jambo linalo pelekea kuharibu huduma za matibabu.

Kisha yakazungumzwa makosa ya kitabia ambayo hufanywa na baadhi ya madaktari na yanayoweza kuepukwa, kwa kuwafundisha maadili ya udaktari na kuhakikisha yanafanyiwa kazi.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed hufanya warsha na kutoa mihadhara ya kielimu mara kwa mara, kinamkakati wa kuendeleza watumishi wake, kimalezi na kielimu na kuwafanya waweze kufanya tafiti za kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: