Kutandika uwanja wa katikati ya haram mbili kwa mamia ya miswala kila siku na idadi huongezeka katika simu za ziara

Maoni katika picha
Idara ya kutandika miswala chini ya kitengo cha uwanja wa katikati ya haram mbili, hutandika makumi ya miswala kwenye uwanja huo na sehemu zilizo pauliwa kila siku, na huongezeka idadi ya miswala kutokana na kuongezeka kwa mazuwaru katika siku za ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu au usiku wa Ijumaa, watumishi wa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) huanza maandalizi mapema kwa ajili ya kuhakikisha ibada ya ziara na dua inafanywa kwa urahisi.

Kiongozi wa Idara Sayyid Muhammad Ali Mussa ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa idara wanafanya kazi kubwa kuhakikisha ibada ya swala na ziara inafanywa kwa urahisi ndani ya uwanja wa katikati ya haram mbili sehemu ambayo hutumiwa na mazuwaru wengi kama sehemu ya kupumzika, kutokana na hali ya hewa sehemu hiyo huwa mahala muwafaka kwao, hivyo hutandikwa sehemu kubwa ya eneo hilo hususan usiku wa Ijumaa ambao hushuhudiwa idadi kubwa ya mazuwaru”.

Akaongeza kuwa: “Miswala iliyo tandikwa inaurefu wa (mt 6) na upana mita moja, katika siku za kawaida hutandikwa miswala (200) lakini katika usiku wa Ijumaa na siku za ziara maalum hutandikwa miswala hadi (800)”.

Akaendelea kusema: “Kazi hii hufanywa kila siku mara tatu, sambamba na kuchukua jukumu la kutunza usafi wa miswala iliyo tandikwa ndani ya uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu, kila baada ya muda miswala hutanduliwa na kupelekwa kuoshwa, pamoja na kazi ya utoharishaji wa haraka ambao hufanywa kwa kutumia vifaa maalum vidogo vidogo vya umeme mara tu baada ya mswala kunajisika”.

Akafafanua kuwa: “Sehemu inayo tandikwa imekadiriwa vizuri ulefu na upana kwa namna ambayo haitatizi harakazi za mazuwaru, kazi ya kutandika hufanywa kwa muda maalum, tunahazina kubwa ya miswala inayo tosha kutandika eneo linalo hitajika kulingana na idadi ya mazuwaru”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: