Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Hilla ni mji mtukufu uliotunza elimu na maarifa ya Ahlulbait (a.s)

Maoni katika picha
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi amesema kuwa: “Mji wa Hilla ni miongoni mwa miji mitukufu inayotunza elimu na maarifa ya Ahlulbait (a.s), na unaumuhimu mkubwa katika turathi za Iraq kwa ujumla, na katika dini za Mwenyezi Mungu, mji wa Hilla unahistoria iliyo andikwa na mamia ya waandishi wa historia ndani ya vitabu vya historia, adabu, rijali na jografia”.

Akabainisha kuwa: “Katika mji huo kunachuo kikongwe zaidi nacho ni kitovu cha elimu tofauti, kama vile historia, fiqhi, usulu, rijali, adabu, na elimu zingine nyingi, aidha mji huo umetoa wanachuoni wakubwa, kama vile Ibun Idrisa Alhilliy, muhaqiqu Alhilliy, Alammah Alhilliy, Ibun Twausi na wengine wengi, hivyo Atabatu Abbasiyya ikaona kuna umuhimu wa kuanzisha kituo rasmi cha kuhuisha turathi hizo na urithi wa kielimu na kimazingira nacho ni kituo cha turathi za Hilla kinacho fanya kazi ya kufichua hazina hiyo ya elimu na kuiweka kwenye nuru”.

Ameyasema hayo alipo tembelea kituo hicho akiwa pamoja na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Liith Mussawi, na Shekh Ali Asadi makamo rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu.

Kumbuka kuwa ziara ilikuwa kwa ajili ya kukagua kazi na kuangalia maendeleo ya uandishi wa vitabu na uhakiki pamoja na kuangalia mwenendo wa kazi wa jarida mbili zinazo chapishwa na kituo hicho, hali kadhalika makamo katibu mkuu ametoa ujumbe elekezi kwa watumishi wa kituo hicho, ameeleza haki za watumishi na mfumo wa taasisi unaofuatwa na Ataba tukufu, unaosaidia kufikia malengo ya kila kituo kilicho chini yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: