Kufanya majlisi za kuomboleza ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya kuomboleza iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika tukio hili la kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kuna vipengele vingi kikiwemo hiki cha kufanya majlisi za kuomboleza.

Miongoni mwa majlisi hizo pia ni hii ambayo hufanywa kila mwaka na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Ataba tukufu, hudumu siku tatu kwa kufanya majlisi mbili kila siku asubuhi na jioni, hujikumbusha kifo cha bibi Zaharaa (a.s), na misiba aliyopitia baada ya kuondokewa na baba yake Mtume Muhammad (s.a.w.w), hadi akaondoka duniani na kuacha majonzi makubwa katika nyoyo za wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) majonzi yasiyo isha na wataendelea kurithishana kizazi baada ya kizazi.

Majlisi ya asubuhi hufanywa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na mzungumzaji huwa ni Shekh Ali Khafaji, na majlisi ya jioni mzungumzaji ni Shekh Najahu Ramithi huhitimisha majlisi hizo kwa kaswida ambazo huimbwa na Ali Basha.

Wazungumzaji wameeleza mafundisho mema kutoka katika historia ya bibi Zaharaa (a.s) na namna ya kunufaika nae kama taa liangazalo kwa kila mtu, hakika yeye ni shule kamili inayo enda sambamba na zama zote wala haipitwi na wakati.

Kumbuka kuwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia wanaomboleza msiba huu wa kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s), kunariwaya tofauti kuhusu tarehe ya kifo chake na sehemu lilipo kaburi lake (a.s), hii inaonyesha ukubwa wa dhulma aliyo fanyiwa, iliyo mpelekea atoe usia kwa mume wake kiongozi wa waumini Ali (a.s), afiche sehemu ya kaburi lake na wala jeneza lake lisishuhudiwe na yeyote katika waliomdhulumu haki yake, wakati anafariki alikuwa na umri wa miaka kumi na nane kwa mujibu wa riwaya mashuhuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: