Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake imeanza kutoa semina za Quráni mkoani Bagdad na kwenye mikoa mingine

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza kutoa semina kwa njia ya mtandao kwenye matawi yake ya (Bagdad – Dhiqaar – Diwaniyya) inahusu usomaji sahihi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.

Hayo yamesemwa na kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi, akaongeza kuwa: “Tunatarajia kutoa semina kumi kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (Google Meet) nazo ni sehemu ya kuendeleza harakati za Maahadi za kusambaza utamaduni wa kufuata mafundisho ya Quráni, katika jamii hususan kwa wanawake”.

Akaongeza kuwa: “Semina zitajikita katika ufundishaji wa Quráni kwa njia rahisi kwa wanao anza, wanafunzi tumewagawa kwenye makundi kutokana na umri pamoja na viwango vyao vya elimu, wakufunzi wa semina hizo wanauzowefu mkubwa”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tawi la wanawake imezowea kufanya harakati mbalimbali kila mwaka, zikiwemo semina hizi za Quráni tukufu, lakini kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa na tahadhari ya kujikinga na maradhi ya virusi vya Korona, mwaka huu tumetosheka kwa kufanya harakati chache ikiwemo hii ya kutoa semina kwa njia ya mtandao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: