Kwa lengo la kubadilishana uzowefu: ugeni kutoka Atabatu Alawiyya umetembelea miradi kadhaa ya Atabatu Abbasiyya

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Alawiyya takatifu kupitia kitengo cha kilimo na ufugaji wametembelea baadhi ya miradi ya Atabatu Abbasiyya, ya kilimo, ufugaji na viwanda, kwa lengo la kuangalia shughuli za uzalishaji, sambamba na vifaa vya kisasa vinavyo tumika katika miradi hiyo.

Ugeni huo umesikiliza maelezo kutoka kwa wasimamizi wa miradi hiyo ambao wamefafanua kuhusu uzalishaji na vifaa vya kisasa wanavyo tumia, pamoja na malengo yaliyotimizwa na miradi hiyo ambayo yamenufaisha raia wa Iraq na soko la ndani.

Tumeongea na rais wa kitengo cha kilimo na mifugo katika Atabatu Alawiyya takatifu Mhandisi Mustwafa Muhammad Ali amesema kuwa: “Ugeni wetu umejumuisha viongozi wa idara na wakuu wa vitengo pamoja na wataalamu wa kilimo na mifugo, lengo la ziara yetu ni kuangalia maendeleo kwenye miradi hiyo na mbinu za kisasa zinazo tumika katika uzalishaji, ikiwa ni pamoja na umwagiliaji wa kisasa na mbinu zingine”.

Akaongeza kuwa: “Tumetembelea mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi (a.s), mradi wa Saaqi, mradi wa Firdaus, mradi wa Awali, mradi wa ufugaji kware, ufugaji wa n’gombe pamoja na shirika la Khairul-Juud na shirika la uchumi Alkafeel”.

Akaendelea kusema: “Kupitia ziara hii tunatarajia kubadilishana uzowefu kati ya watumishi wetu na watumishi wa miradi hiyo ili kuporesha uzalishaji katika kilimo na ufugaji kwa faida ya taifa na wananchi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: