Kuimarisha ushirikiano wa kimalezi: ugeni kutoka muungano wa vituo vya malezi vya kiiraq umetembelea Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Ugeni kutoka muungano wa wasimamiaji wa vituo vya malezi vya Iraq wametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, na kukutana na viongozi wengi, kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano wa kimalezi baina ya pande mbili.

Ziara hii imefanywa kwa ushirikiano na idara ya uhusiano wa vyuo vikuu na shule chini ya kitengo cha uhusiano katika Ataba tukufu.

Kuhusu ziara hiyo tumeongea na kiongozi wa idara ya harakati za shule bwana Mahmuud Qarrah Ghuli amesema kuwa: “Ugeni kutoka muungano wa vituo vya malezi vya kiiraq ukiwa na wajumbe (25) kutoka mikoa tofauti ya Iraq umetembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuangalia namna ya kuimarisha ushirikiano wa kielimu baina yao”.

Akaongeza kuwa: “Ugeni umeongea mambo mengi kuhusu ratiba za kielimu na kimalezi, na umeonyesha Imani yao kwa Ataba tukufu kuwa iko tayali kusaidia miradi ya elimu hapa Iraq, aidha ugeni huo umejadili swala la ufundishaji hapa nchini, ni matarajio yetu wafanye ziara tena kama hii siku za mbele kwa ajili ya kuangalia matunda ya ushirikiano huu”.

Kumbuka kuwa idara ya uhusiano wa vyuo vikuu na shule chini ya kitengo kikuu cha Atabatu Abbasiyya hufanya makongamano na harakati mbalimbali kwa kushirikiana na vyuo vya Iraq ndani ya kipindi chote cha mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: