Multaqal-Qamaru wanajadiliana na chuo cha Imamu Al-Kaadhim (a.s) kuhusu uhusiano wa kitamaduni na kielimu

Maoni katika picha
Ugeni kutoka kituo cha utamaduni Al-Qamaru chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, umetembelea chuo cha Imamu Al-Kaadhim (a.s) kwa ajili ya kufungua milango ya ushirikiano wa kitamaduni na kielimu baina yao, kwa manufaa ya wanafunzi wa chuo chini ya ratiba ya kituo.

Tumeongea na Shekh Haarith Daahi kuhusu ziara hiyo amesema kuwa: “Ni sehemu ya utaratibu wa kituo ulio andaliwa katika mkoa wa Bagdad na umefunguliwa kwa ziara hii, kulikuwa na kikao kilicho tukutanisha na Dokta Muhammad Waadhihi na makamo wa kitengo cha elimu, pamoja na kundi la walimu na marais wa vitengo na wajumbe wa kamati ya chuo, tumejadili namna ya kutumia ratiba ya chuo inayo lenga kulea vijana kwa mada za kitamaduni, na umesha wekwa mkakati wa shughuli hiyo katika chuo”.

Dokta Muhammad Waadhihi akafafanua kuwa: “Hakika uhusiano mzuri uliopo kati ya chuo na Ataba takatifu unasaidia kuwepo na kazi nyingi za kushirikiana, katika sekta tofauti na vituo mbalimbali, katika mambo ya kielimu na kitamaduni, miongoni mwa vipao mbele vya uhusiano wetu na Ataba takatifu ni kuratibu makongamano na warsha za kielimu pamoja na nadwa, na kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa chuo katika mkoa wa Bagdad kupitia taasisi za Ataba takatifu kulingana na fani ya kila kitengo”.

Mwisho wa mkutano wao wakatoa wito wa kuongeza ushirikiano na kuingia katika hatua ya utekelezaji wa makubaliano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: