Maahadi ya Quráni tukufu imeratibu mhadhara wa msimamo wa kiislamu kuhusu unafiki katika Quráni na kutumia khutuba ya bibi Zaharaa (a.s) kama mfano

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia tawi lake la Najafu, imeratibu mhadhara wa msimamo wa kiislamu kuhusu unafiki katika Quráni na Sunna.. na kutumia khutuba ya (bibi Zaharaa (a.s) kama mfano) mhadhara umetolewa na mwalimu wa hauza Sayyid Hussein Hakiim.

Ameongea mambo mengi yenye uhusiano na mada, akaonyesha hatari ya unafiki na wanafiki kama inavyotajwa ndani ya Quráni tukufu, ambapo Mwenyezi Mungu amewaahidi udhalili na fedheha pamoja na adhabu kali, kuna sura kalimi inaitwa surat Munafiqina kwa ajili ya kuwatahadharisha waumini na unafiki.

Mhadhara ukahitimishwa kwa utenzi kuhusu msiba mkubwa aliopata bibi Zaharaa (a.s), na mambo yaliyo jiri baada ya kifo cha baba yake Mutume Muhammad (s.a.w.w).

Kumbuka kuwa majlisi hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa Maahadi katika mkoa wa Najafu, inafanywa kwa mwaka wa tatu mfululizo, na kuhudhuriwa na kundi kubwa la wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) pamoja na watumishi wa kitengo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: