Ofisi ya Marjaa Dini mkuu imetoa fatwa ya kujuzisha kutumia chanjo ya virusi vya Korona iliyo pasishwa na madaktari bingwa

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu siku ya Jumatatu mwezi (11 Jamadal-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (25 Januari 2021m) imetoa fatwa ya kujuzisha matumizi ya chanjo ya virusi vya Korona zilizo tengenezwa na mashirika mbalimbali, baada ya kupokea swali kutoka kwa watu wanaoishi Landan, na ifuatayo ni nakala ya swali hilo.

Swali kutoka kwa watu wanaoishi Landan likielekezwa katika ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu ampe afya njema na umri mrefu Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Sistani, ni matumaini yetu mheshimiwa Marjaa Dini mkuu utatupa ufafanuzi wa maswali yafuatayo:

  • 1- Shirika la Faiza (nchini Marekani) limetangaza kuwa limefanikiwa kutengeneza chanjo ya virusi vya Korona, pamoja na shirika la Istarazinka (la Ulaya) na hivi karibuni zitatangazwa chanjo zilizo tengenezwa na mashirika mengine kutoka nchi tofauti duniani, pamoja na kuwepo kwa baadhi ya matokeo mazuri ya chanjo hizo na idara za afya za nchi mbalimbali zimeruhusu kutumia chanjo hizo, na utaratibu wa utumiaji wake umetangazwa kote duniani, lakini baadhi ya wafuasi wako wanapata dhiki kutumia chanjo hizo, kwa sababu hatua za majaribio yake –zilikua tofauti na chanjo zilizo zoweleka- zimeruhusiwa haraka kabla ya kufika hatua ya mwisho, serikali nyingi zimeruhusu kutumika chanjo hizo katika mazingira ya dharura, na baadhi ya watu wenye asili ya Iraq wanaogoga kuzitumia kutokana na mambo yaliyowahi kutokea zamani, hawana Imani na chanjo hizo, lakini bado hayajashuhudiwa madhara makubwa yanayo tokana na chanjo hizo, katika mazingira haya ofisi yako inashauri nini?
  • 2- Serikali nyingi zimewapa kipaombele zaidi ya kuanza kupewa chanjo hiyo watumishi wa afya na watu wenye umri mkubwa na askari, aidha kuna watu wanalipa pesa ili wapewe chanjo hiyo kabla ya makundi tuliyotaja hayajamaliza, je kuheshimu utaratibu uliopangwa katika utowaji wa chanjo ni wajibu kisheria?
  • 3- Je ofisi yako inaruhusu –iwapo madaktari watapasisha kutumia chanjo hiyo- kutumika pesa ya haki za kisheria kununua chanjo ya Korona na kuigawa kwa wahitaji ndani na nje ya nchi, kutokana na kushindwa kumudu gharama ya chanjo hiyo kwa baadhi ya nchi zinazo julikana kama ulimwengu wa tatu, nchi hizo imma haziwezi kununua chanjo inayo tosha raia wake wote, au haziwezi kununua chanjo itakayo tosha raia wote ndani ya muda muwafaka au raia wake hawana uwezo wa kumudu gharama ya chanjo hiyo?
  • 4- Iwapo mashirika yanayo tengeneza chanjo yakitoa wito wa kupatikana watu watakao jitolea kufanyiwa majaribio ya chanjo ili kufahamu uwezo wake, je inaruhusiwa waumini kujitolea? Pamoja na kuwepo mkataba (bima) ya kulinda afya ya mtu alitakaejitolea, lakini pamoja na kuwepo kwa hatari ya kupata madhara maishani kutokana na majaribio hayo?
  • 5- Katika utumiaji wa chanjo hiyo hutumika vitu vingi ikiwa ni pamoja na sampo za nguruwe, je inatosha wao kutosema kama wametumia sampo za nguruwe, au kusema kama hawajatumia, japo kuwa inajulikana kuwa sampo za nguruwe hutumika kwenye chanjo nyingi japo kuwa hukumu ya kubadilika inawezekana kwenye chanjo, je ni lazima kuchunguza swala hilo? Japokuwa mtumiaji anaweza kuwa na wasiwasi ya kuruhusiwa kutumia chanjo hiyo kwa dharura?

Jibu:

  • 1- Katika mazingira hayo inatakiwa kuzingatia ushauri wa madaktari wenye uzowefu na mambo hayo, kuhusu upande wa sheria ni wajibu kutumia chanjo iliyopasishwa kuwa inauwezo wa kuzuwia virusi vya Korona, na haifai kujiingiza katika hatari inayotishia uhai wa mtu au kupata madhara makubwa yasiyoweza kuzuwilika kutokana na utumiaji wa chanjo.
  • 2- Haifai kuvunja utaratibu ikiwa ni kwenda tofauti na sheria.
  • 3- Hakuna shida kufanya hivyo katika mazingira ya dharura.
  • 4- Haifai kufanya hivyo inapokua kuna tishio la uhai, au matarajio ya kupata madhara makubwa ambayo ni vikumu kuyaepuka, lakini utakapokua uwezekano wa kupata madhara ni mdogo na hauzingatiwi basi itafaa.
  • 5- Hakuna tatizo kisheria.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: