Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlisi za kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s)

Maoni katika picha
Kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Ummul-Banina (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi maalumu ya kuomboleza, ni utamaduni uliozoweleka wa kuomboleza siku za huzuni kwa watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya, imefunguliwa kwa Quráni kisha ukafuata mhadhara wa kidini uliotolewa na Shekh Muhsin Asadi kutoka kitengo cha Dini, amezungumza mambo mengi kuhusu maisha ya Ummul-Banina (a.s), mama aliyejua utukufu wa Ahlulbait (a.s), akaeleza msimamo wake katika vita ya Twafu pale alipo watoa watoto wake wanne kwenda kumnusuru Imamu Hussein (a.s) na kuuwawa kwa ajili ya kumlinda Imamu wa zama zao na kupigania Dini ya Mwenyezi Mungu mtukufu.

Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma qaswida iliyo eleza maumivu wanayopata wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kufuatia msiba huo.

Kumbuka kuwa siku ya mwezi kumi na tatu Jamadal-Aakhar ni kumbukumbu ya kifo cha bibi mtakatifu Ummul-Banina (a.s), naye ni Fatuma bint Hizaam bun Rabia Alkilabi, Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: