Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza tarehe ya kufanywa kongamano la Imamu Baaqir (a.s) la kitamaduni awamu ya saba

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kutunza urithi na utamaduni wa Ahlulbait (a.s) kutokana na umuhimu wake kwa binaadamu, katika kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Baaqir (a.s), kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza kufanya kongamano la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya saba chini ya kauli mbiu isemayo (Imamu Baaqir –a.s- ni mtu mtakatifu na kilele cha utukufu) mwezi mosi Rajabu mwaka 1442h sawa na tarehe (14/02/2021m).

Mjumbe wa kamati ya maandalizi na rais wa kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Aqiil Abdulhussein Alyaasiri amesema kuwa: “Kongamano linafanywa kwa mwaka wa saba mfululizo, tayali tumeshafanya vikao vingi vya kujadili maandalizi ya kongamano la Imamu Baaqir (a.s), tumejadili ratiba ya kongamano hilo na malengo yake pamoja na mada zitakazo wasilishwa, ili kuhakikisha zinaendana na malengo ya kongamano hilo, linalo tarajiwa kufanywa mwezi mosi Rajabu 1442h Insha-Allah.

Akaongeza kuwa: “Kamati inayo simamia kongamano hilo imeangazia sekta muhimu za kielimu zinazo endana na utukufu wa mtu ambaye kongamano limebeba jina lake, hili ni jukumu kubwa sana kwa kamati ya maandalizi, kwani Imamu Baaqir (a.s) ndiye chemchem ya elimu za fikra na itikadi.

Akasema: “Miongoni mwa malengo ya kongamano hili ni kufikisha ujumbe kwa kila mfuasi wa Ahlulbait (a.s) na kutoa mafundisho ya Mwenyezi Mungu ambayo kama umma ukishikamana nayo hautapotea milele”.

Kumbuka kuwa kongamano la Imamu Baaqir (a.s) ni miongoni mwa makongamano ambayo hufanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, katika kuhuisha kuzaliwa kwa Imamu Baaqir (a.s) na kuangazia nafasi ya pekee aliyokuwa nayo, na kufanyia kazi mafundisho ya kimalezi na kibinaadamu aliyo fundisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: