Maahadi ya Quráni tawi la Najafu tukufu inahitimisha kikao cha usomaji wa Quráni

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu/ tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya imemaliza kikao cha usomaji wa Quráni, washiriki wa kikao hicho wamepewa majaribio mengi, ili kuwaandaa vizuri baada ya kuhitimu kwao, na kwenda kusambaza walicho soma katika miji yao.

Mkufunzi alikua ni Dokta Karim Jabri Zubaidi mbobezi wa fani ya Tajwidi, ametumia njia ya mawasiliano ya kijamii kuwasiliana na wanafunzi wake na kuwaimarisha katika usomaji wa Quráni, alikua anatumia mawasiliano ya kuonekana (video call) kwa sababu urekebishaji wa matamsi unahitaji kuangalia kwa usahihi namna ya utamkaji wa herufi.

Kumbuka kuwa kikao hiki ni sehemu ya harakati nyingi zinazo fanywa na Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, kupitia matawi yake tofauti kwa ajili ya kueneza utamaduni ya kusoma Quráni katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: