Mawakibu za Husseiniyya: zinaendelea kusaidia wenye mahitaji

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili takatifu, kimesema kuwa mawakibu Husseiniyya zilizo chini yake zinaendelea kusaidia familia za mafakiri na wenye kipato kidogo, ambazo zimeathirika na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa ya janga la virusi vya Korona, jambo lililo ongeza ugumu wa maisha katika familia hizo, utoaji wa misaada hiyo ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kusimama pamoja na familia hizo na kuzisaidia.

Miongoni mwa mawakibu hizo ni hii yenye jina la (Imamu Hussein –a.s-) kutoka Bagdad, ambayo inaendelea kutoa misaada kwa familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, msafara wa kugawa misaada uliofanywa hivi karibuni ni moja ya misafara mingi wanayo fanya, kiongozi wa maukibu hiyo bwana Maitham Bahadeli amesema kuwa: “Maukibu yetu ni sawa na mawakibu zingine za Husseiniyya katika mji wa Bagdad au sehemu zingine, tunaendelea kusaidia familia za watu wanaishi katika mazingira magumu, safari hii tumeandaa vifurushi (100) vya chakula vikavu na vilivyo pikwa, pamoja na vitu vingine kama vile nguo na vifaa vya umeme kulingana na mahitaji ya kila familia iliyo kubali kupokea hiki kidogo tunacho wapa, ni matumaini yetu kitawasaidia japo kidoga katika maisha yao”.

Rais wa kitengo hicho bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan amesema kuwa: “Hakika mawakibu za Husseiniyya zinazo toa huduma zimeanza opresheni kubwa ya kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo walio athirika na janga la virusi vya Korona, tangu siku ya kwanza ambayo Marjaa Dini mkuu alitoa wito huo, hili ni deni la mawakibu hizi ambazo zimekua mstari wa mbele kupambana na kila tatizo linalo tokea Iraq, mara ya mwisho zilisimama imara dhidi ya magaidi wa Daeish, zikatoa mchango mkubwa katika kufanikisha ushindi na kukomboa ardhi ya Iraq”.

Kumbuka kuwa Marjaa Dini mkuu alitoa wito wa kushirikiana na kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, wakati wa marufuku ya kutembea iliyo wekwa kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, ndio Atabatu Abbasiyya tukufu ikaanzisha program ya (Marjaiyyatu-Takaaful) kwa ajili ya kuzitambua na kuzisaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo walio athiriwa na marufuku hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: