Kuanza hatua ya pili ya semina ya watumishi wanaojitolea kufuatilia adabu za ziara

Maoni katika picha
Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeingia hatua ya pili ya semina yake maalum kwa watumishi wa kujitolea katika idara ya adabu za ziara, chini ya ofisi ya tabligh katika kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika utendaji wao, kulingana na majukumu yao.

Kiongozi wa idara hiyo Sayyid Hassan Aáraji ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika hatua hii ni sehemu ya kukamilisha hatua ya kwanza, tunajumla ya washiriki (60) kutoka mikoa tofauti chini ya utaratibu maalum uliowekwa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, kinacho simamia semina hii kupitia zamu mbili, kila zamu inawashiriki (30)”.

Mkufunzi wa semina Ustadh Ali Shimri amesema kuwa: “Miongoni mwa mambo yaliyo fundishwa awamu hii ni (diplomasia ya maongezi) na ilikua na mada tofauti, ikiwemo mada isemayo (umuhimu wa maongezi yenye tija na njia za kujenga maelewano, aina za watu na jinsi ya kuamiliana nao, masharti na aina za maongezi, vikwazo vya maongezi, njia za kuathiri)”.

Naye mkufunzi wa warsha ya (kuchunga muda na vipaombele) Dokta Ahmadi Dakhal Jabasi akasema: “Warsha ilikuwa na mada nyindi, miongoni mwake ni (kuchunga muda na vipaombele vyake, matatizo ya kutochunga muda, mkakati wa kuwa na ratiba ya majukumu ya kila siku, umuhimu wa kuwa na ratiba ya kila wiki)”.

Kumbuka kuwa watumishi hawa wa kujitolea wamechaguliwa kuja kusaidia majukumu ya idara hiyo, katika ziara ambazo hushuhudiwa idadi kubwa za mazuwaru katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama vile ziara ya Arubaini, Ashura, Shaábaniyya, arafa, siku za Ijumaa na zinginezo, mafunzo haya yanalenga kuboresha utendaji wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: