Uzalishaji wa mazao bora.. mradi wa Firdaus unaendelea kuingiza sokoni viazi mbatata kwa ajili ya chakula na viwanda

Maoni katika picha
Mradi wa kilimo Firdaus amboa ni miongoni mwa miradi muhimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, unalenga kuingiza sokoni mazao ya kimkakati, umefanikiwa kuzalisha viazi mbatata vingi kwa ajili ya chakula na viwanda, sambamba na kuingiza katika soko la ndani, ifahamike kuwa bidhaa hiyo ni muhimu kwa chakula sawa na ngano na mchele.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa shirika la Liwaau Al-Aalamiyya chini ya Atabatu Abbasiyya na mtekelezaji wa mradi huu Mhandisi Aadil Maalik, amesema: “Mradi wa kilimo Firdaus ni moja ya miradi muhimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye sekta ya kilimo na upatikanaji wa mazao ya ndani, baada ya taifa kushuhudia upungufu mkubwa wa mazao kutoka nje ya taifa, Ataba imesimama imara kuziba pengo hilo kupitia miradi yake tofauti, miongoni mwake ni huu mradi wa kilimo Firadausi katika uzalishaji wa viazi mbatata vya chakula na viwanda”.

Akaongeza kuwa: “Mradi unaendeshwa kwenye shamba lenye ukubwa wa dunam (1183) sehemu ya mazao yake ni viazi mbatata, vinavyo sambazwa kwa makampuni ya kitaifa yanayo husika na ukusanyaji wa zao hilo, na sehemu ya pili vinasambazwa masokoni kwa ajili ya chakula kwa raia, tumefanikiwa kupata mavuno makubwa ya viazi vyenye ubora mkubwa ukilinganisha na viazi vilivyopo sokoni, na vimesaidia kujitosheleza katika sekta hiyo, sambamba na kuwa na uhakika wa chakula”.

Akaendelea kusema: “Mradi haujaishia kwenye kilimo hicho peke yake, bali kuna mazao mengine kama inavyo pangwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kunufaika na uzowefu wetu pamoja na njia za kisasa za kilimo hicho na vingine, sambamba na kuchangia katika kutatua tatizo la ajira na kuboresha mazingira kwa kubadilisha jangwa kuwa kijani kibichi”.

Mkuu wa mradi huo Mhandisi Haidari Dahani amesema: “Mazao yetu yanaubora mkubwa na uwezo wa kukaa muda mrefu bila kuharibika pia hayana bakteria kwani husamadiwa kwa mbolea bora kutoka shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Khairul-Juud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ni aina pekee ambayo inazalishwa katika mradi huu”.

Akamaliza kwa kusema: “Hakika bidhaa zetu zinazo zalishwa kwa ajili ya viwanda au chakula huthibitishwa na maabara za kupima ubora, wakati wote zimekutwa na ubora mkubwa, tunatarajia kuongeza uzalishaji baada ya mafanikio yaliyopatikana katika shamba hili, siku za nyuma ilikua vigumu kulima jangwani na kupata mavuno makubwa kiasi hiki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: