Warsha ya kujenga uwezo kwa watumishi wa kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeandaa warsha yenye anuani isemayo (Uongozi bora) kwa watumishi wake ili kuboresha utendaji wao na utekelezaji wa majukumu yao.

Watahudhuria masomo kila siku bila kuathiri ratiba zao za kazi na kwa kufuata ratiba maalum ya masomo chini ya walimu mahiri waliobobea kwenye sekta hiyo, watafundishwa kwa awamu hadi wafikiwe watumishi wote wa kitengo hicho.

Mkuu wa kituo cha mafunzo ya habari Ustadh Ali Kaabi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: Hii ni hatua ya kwanza ya mafunzo ya utawala bora, na tumeanza na kufundisha maana ya ubora pamoja na kuangalia mifano ya kihistoria ya neno hilo na jinsi linavyo eleweka kimataifa.

Akaongeza kuwa: Watapewa mafunzo haya watumishi wote wa kitengo hiki na yatakua na mambo mengi siku za mbele.

Akasema: Lengo la mafunzo haya ni kutaka kwendana na ubora wa kimataifa katika utekelezaji wa majukumu sambamba na kutambua namna ya kujikinga na milipuko.

Ustadh Zamaan Faraji Jaasim mkufunzi wa warsha hiyo amesema: “Hakika utawala bora husaidia kutekeleza majukumu na kutoa huduma nzuri”.

Akaongeza kuwa: “Kupitia mada ya utawala bora tunajifunza uwelewa wa aina za ubora na mambo ya msingi yanayo husiana na ubora, pamoja na nafasi ya utawala bora kwenye nyanja zote”.

Akamaliza kwa kusema: “Baada ya warsha hii washiriki wataweza kutoa huduma bora na kufafanua uwelewa mbalimbali wa ubora kama unavyo elezwa na wadau wa ubora, na wataweza kuboresha utendaji wao katika taasisi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: