Kusafisha, kuweka marashi na kutandika miswala mipya katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa mbora wa wanawake Fatuma Zaharaa (a.s), haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imesafishwa, kutiwa marashi na kutandikwa miswala mipya, kazi hiyo imesimamiwa na idara ya usimamizi wa haram tukufu na baadhi ya watumishi wengine wa malalo hiyo takatifu.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara hiyo bwana Nizaar Ghina Khaliil amesema: “Usiku wa jana baada ya kupungua mazuwaru, tulifunga milango ya haram na kutandua miswala ya zamani halafu tukadeki na kuosha kuta, milango na madirisha kwa kutumia vifaa maalum”.

Akaongeza kuwa: “Tumeosha dirisha la malalo takatifu kwa kutumia vifaa maalum vinavyo saidia kuhifadhi ubora wake, kisha tukapuliza marashi yenye ubora mkubwa, halafu tukatandika miswala mipya kwa kufuata vipimo maalum, miswala iliyo tandikwa ni ya kifahari na rangi zake zinaendana na rangi za miswala ya haram takatifu”.

Kumbuka kuwa watumishi wa idara hiyo wanajukumu la kutoa huduma ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na eneo la pambo la dhahabu lililopo upande wa Kibla, wanasimamia matembezi ya mazuwaru kwenye ziara za kawaida au kubwa, na kuhakikisha hakutokei msongamano ndani na nje ya haram takatifu, pia wanajukumu la kudumisha usafi sehemu zote za haram hadi kwenye mapambo, milango, taa, viyoyozi na vitu vingine vinavyo fanya malalo iwe na muonekano mzuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: