Kuweka muonekano wa furaha na mapambo katika Atabatu Abbasiyya tukufu kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa bibi Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Katika kuadhimisha kuzaliwa kwa mtoto wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w) mbora wa wanawake Fatuma Zaharaa (a.s), muonekano wa furaha na mapambo mazuri yametanda kwenye kuta na korido za malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hakika ni kumbukumbu ambayo ulimwengu mzima umejaa furaha, kwa kuzaliwa kwake ardhi na mbingu zimenawirika kwa nuru yake na Mola wake kamfanya kuwa zao jema.

Kuta na korido za Ataba takatifu zimewekwa mapambo na mabango yaliyo andikwa maneno mazuri ya pongezi, na zimewashwa taa za rangi ambazo ni maalum kwa ajili ya matukio ya furaha, pamoja na kuweka mauwa na miti katika milango ya haram na maeneo mengine ndani ya haram takatifu.

Hali kadhalika Atabatu Abbasiyya imejiandaa kupokea mazuwaru watakao kuja katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kutoa pongezi kwa tukio hili tukufu katika nyoyo za wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), Ataba imeandaa ratiba maalum ya kuadhimisha tukio hilo takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: