Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu kinafanya tamasha la uimbaji wa mashairi katika kumbukumbu ya kuzaliwa Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu chini ya Atabatu Abbasiyya jioni ya Jumatano, kimefanya tamasha la kuimba mashairi katika kuadhimisha kuzaliwa kwa mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s).

Waimbaji wa mashairi na tenzi za Husseiniyya wameshiriki kwenye tamasha hilo, wamepaza sauti zao zilizojaa mapenzi kwa Batuli mtakatifu na familia yake (a.s), tamasha hilo limepambwa na vitu vingine pia.

Tumeongea na rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi kuhusu kongamano hilo, amesema: “Hakika kongamano hili lipo katika mpango-kazi wa mwaka, ulio andaliwa na kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wa kufanya mahafali na majlisi katika matukio ya kuzaliwa na kufariki kwa Maimamu watakasifu (a.s) pamoja na watu wengine muhimu katika familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.

Akaongeza kuwa: “Kitengo chetu kinalipa uzito swala la kuadhimisha mambo yaliyo tokea katika nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), kupitia matamasha ya uimbaji wa mashairi na maonyesho, tumezowea kufanya hivyo kila mwaka”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: