Nadwa kuhusu tabia za bibi Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa nadwa yenye anuani isemayo: (Maadili ya familia kwa bibi Fatuma Zaharaa –a.s- katika hadithi kisaa), mhadhiri wa nadwa hiyo ni Dokta Kawakibu Fadhili rais wa kitengo cha maarifa ya Quráni na malezi ya kiislamu katika kitivo cha Tarbiyya/ chuo kikuu cha Kufa.

Kufanyika kwa nadwa hii ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zaharaa (a.s) na kuangazia mafundisho kutoka katika mwenendo wake mtakatifu na hatua za maisha yake.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi amefafanua kuwa: “Hakika nadwa hii ni sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mbora wa wanawake wa duniani bibi Fatuma Zaharaa (a.s), mwanamke wa mfano ambaye yatupasa kusoma historia yake na kufuata mwenendo wake, ili kufanya maisha yetu ya familia kuwa bora, hakika yeye ni nuru ingáayo, tujifunze kutoka kwake misingi ya mafanikio na utulivu wa familia”.

Akaongeza kuwa: “Mhadhiri ameongea mambo muhimu kuhusu uhai wa bibi Zaharaa (a.s) katika upande wa familia, hakika alikua nuru inayoangazia familia za kiislamu, mfano mwema wa tabia zilizo fundishwa ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, hakika Zaharaa (a.s) alikua kielelezo bora cha mwanamke wa kiislamu, akaeleza namna alivyokua anatekeleza majukumu yake kama mama, mke na mlezi wa familia”.

Nadwa imepata muitikio mkubwa pamoja na ushiriki mzuri uliojaa maoni na maswali mbalimbali, naye Dokta Fadhili alijibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi pale ilipo hitajika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: