Atabatu Abbasiyya tukufu imemaliza kuandaa faharasi na kuweka vitabu vya maktaba kongwe katika mji wa Karbala

Maoni katika picha
Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimekamilisha kutengeneza shelfu za vitabu na kuweka faharasi ya majina ya vitabu kwenye maktaba ya Jaafariyya katika madrasa ya Hindiyya, ambayo ni moja ya madrasa kongwe katika mkoa wa Karbala, ilianzishwa karne ya tatu hijiriyya, maktaba hiyo inaidadi kubwa ya vitabu vya aina tofauti vinavyo hitajiwa na wanafunzi wa dini.

Mkuu wa madrasa Shekh Abdulhadi Saádi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika kazi iliyofanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kituo cha faharasi na kupangilia taaluma katika maktaba Jaafariyya, wameandaa na kupanga vitabu, mtu yeyote atakaetembelea maktaba anaweza kuchukua kitabu chochote anacho hitaji kwa urahisi, hapo zamani walikua wanapata tabu, shukrani za dhati ziwaendee, na hili sio jambo geni kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, imezowea kufanya kazi hizi ikiwa ni pamoja na sehemu hii ambayo ilijengwa upya mwaka (2008) baada ya kuvunjwa wakati wa maandamano ya Shaabaniyya, na kupafanya kuwa kama zamani na maktaba kurejea kama ilivyokua, hakika huzingatiwa kuwa msingi muhimu kwa wanafunzi wa Dini”.

Akaongeza kuwa: “Kwa ajili ya kuwarahisishia wanafunzi kuchukua vitabu wanavyo hitaji kwa muda mfupi, tumeiomba Atabatu Abbasiyya kupitia kituo cha faharasi na kupangilia taaluma, watengeneze faharasi na kupangilia vitabu sambamba na kuweka namba kwenye kila kitabu, kwa ajili ya kumrahisishia mwanafunzi na watumishi wa maktaba, kwa kweli tunatoa shukrani za dhati kwa kituo cha faharasi na kupangilia taaluma kwa kazi kubwa waliyo fanya, wala jambo hili sio ajabu kwao, wamekua mstari wa mbele katika kufanya mambo ya kheri na yenye manufaa kwenye sekta ya elimu na kwa wanachuoni, aidha tunashukuru kazi kubwa ya ukarabati waliyo fanya, hususan watumishi wa kituo cha faharasi, wamefanya kazi kubwa bila kupumzika”.

Mmoja wa wasimamizi wa kazi hiyo Ustadh Ali Twalib Kaadhim kutoka kituo cha faharasi na kupangilia taaluma ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Pamoja na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, watumishi wetu walianza kupanga vitabu vilivyopo maktaba kwa njia za kisasa na kwa kutumia faharasi, kazi hiyo imefanywa kwa hatua zifuatazo:

  • - Kupanga majina ya vitabu kutokana na aina yake kielimu na kimaudhui, baada ya kuwa vilikuwa vimewekwa kwenye shelfu bila mpangilio.
  • - Kupangilia shelfu na kuweka namba kwenye vitabu.
  • - Kurahisisha kazi ya kutafuta kitabu kupitia jina la kitabu, maudhui na muandishi, mpangilio huo unasaidia kupata kitabu chochote kwa haraka bila usumbufu.

Akabainisha kuwa: “Vitabu vimepangwa kisasa kwa utaratibu wa namba, hii ni sehemu ya kazi nyingi zilizo fanywa na kituo, ikiwa ni pamoja na usanifu wa maktaba za umma na binafsi, yote hayo yanafanywa kwa msisitizo wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kusaidia harakati za elimu na utamaduni”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: