Madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel wamefanikiwa kutengeneza matako ya mtoto mwenye miezi kumi

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamefanikiwa kutengeneza matako ya mtoto mwenye umri wa chini ya mwaka mmoja.

Taktari bingwa wa upasuaji wa watoto katika hospitali hiyo Dokta Sarmad Rabii amesema kuwa: “Hakika jopo la madaktari wamefanikiwa kutengeneza uchi wa nyuma wa mtoto mwenye umri wa miezi (10), alikua na tatizo la kukosekana kwa tundu la utumu wa nyuma toka alipo zaliwa”, akabainisha kuwa upasuaji umefanywa kwa hatua moja tu.

Akaongeza kuwa: “Vifaa vya kisasa vilivyopo katika chumba cha upasuaji pamoja na kuwepo kwa jopo la madaktari mahiri, kumetuwezesha kufanya upasuaji huu kwa mafanikio makubwa”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel wakati wote imekua ikitoa huduma bora kupitia vifaa-tiba vya kisasa na madaktari bingwa ilionao kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa tofauti, sambamba na kupokea wagonjwa ambao wapo katika hali mbalimbali za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: