Miongoni mwa hatua za ukarabati wake: Kukamilika kwa kazi ya kuweka marumaru katika mlango wa Imamu Ali Haadi (a.s) kwa ndani

Maoni katika picha
Watumishi wa mradi wa kukarabati mlango wa Imamu Ali Haadi (a.s), uliopo upande wa kaskazini mashariki ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndani, wamekamilisha kazi ya kuweka marumaru kwenye eneo la mlango huo hadi katika haram takatifu.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi hii ni sehemu ya mradi wa kukarabati milango ya haram tukufu (ambayo zamani ilikua ndio milango mikuu), pamoja na mlango mkuu uliopo upande wa nje na kuifanya kuwa kitu kimoja, sambamba na kufuata ramani ya kila mlango kwa namna ambayo inaendana na jengo la Ataba takatifu pamoja na milango mingine”.

Akaongeza kuwa: “Mlango wa Imamu Ali Haadi (a.s) ni mmoja kati ya milango mitatu iliyofaniwa ukarabati, kazi ya kuweka marumaru katika eneo la mlango huo imekamilika na utasaidia kupunguza msongamano wa mazuwaru”.

Akasema: “Kazi iliyobaki katika eneo la mlango huo ni kuweka Kashi-Karbalai kwenye kuta zake, tayali sehemu za kuweka Kashi-Karbalai imesha andaliwa pamoja na mapambo yake”.

Kumbuka kuwa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia miradi mingi iliyo fanywa kwa muda maalum, inayo endana na kila aina ya mradi unaofanywa, kama vile mradi wa upanuzi wa haram katika upauwaji, pamoja na mradi wa kuweka marumaru, ujenzi wa sardabu ndani ya haram na utengenezaji wa dirisha takatifu na kuliweka, sambamba na kuweka mifumo mbalimbali, kama vile mfumo wa viyoyozi, zima moto, tahadhari, mawasiliano, ulinzi na mingineyo, nafasi haitoshi kutaja miradi yote, kila mradi unaumuhimu sawa na mwingine, ukiwemo mradi huu wa kukarabati milango ya malalo takatifu kwa ndani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: