Kuanza kazi ya kuchambulia tende zilizopo eneo la katikati ya haram mbili tukufu

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya mapambo na upandaji wa miti katika kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu wameanza kazi ya kuchambulia tende zilizopandwa katika eneo hilo, kwa ajili ya kuhakikisha ukuaji wake na ubora wa matunda yake pamoja na kuiweka katika muonekano mzuri wa kuvutia.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Haatim Abdulkarim amesema kuwa: “Hakika kazi ya kuchambulia mitende ni moja ya kazi muhimu inayofanywa na idara yetu pamoja na watu wa kujitolea wenye uzowefu na kazi hiyo, hulenga kusafisha mitende na mabaki ya uchafu wa mwaka jana, kama vile kuchambulia matawi na kuondoa makuti makavu, na kuondoa baadhi ya miba ambayo hutatiza upambaji wa tende, aidha husaidia kupunguza maradhi ya tende na kuwa na matunda mazuri yanayo komaa haraka”.

Akaongeza kuwa: “Mitende hii humwagiliwa maji na kuwekwa mbolea ya samadi na ile ya kawaida kutokana na hatua za ukuaji wake, utunzaji wa miti hii ndani ya mwaka mzima hupitia hatua nne, huchambuliwa, na hukomazwa mauwa yake, hatua ya tatu huchambuliwa mauwa na kupunguzwa, na hatua ya nne ndio hii tunayo fanya sasa hivi”.

Kumbuka kuwa mitende imepandwa mistari miwili katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, ni moja ya sehemu muhimu ya kijani kibichi katika eneo hilo, pamoja na umaalum wake, kuna jumla ya miti ya mitende (57) kama ishara ya umri wa Imamu Hussein (a.s) aliyeuwawa kishahidi katika vita ya Twafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: